Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amepinga madai kwamba alikosana na meneja wa klabu hiyo Antonio Conte.
Meneja huyo aliripotiwa kumtaka mchezaji huyo wa miaka 29 kuondoka kabla ya kukamilika kwa siku ya mwisho ya uhamisho lakini Fabregas anahoji kwamba ataendelea kuichezea klabu hiyo hadi mwisho na iwapo atahitajika atajitolea.
Fabregas hatahivyo amechapisha katika mitandao ya kijamii akisema kuwa wawili hao wana uhusiano mzuri na kwamba ataendelea kuichezea Chelsea.
ANTONIO CONTE,MENEJA WA CHELSEA.
No comments:
Post a Comment