Thursday, 11 August 2016

MO BOJAIA YAWASILI DAR KUKIPIGA NA YANGA

Image result for mo bejaia
Kikosi cha jumla ya watu 35 ambao ni wachezaji na viongozi wa MO Bajaia kutoka Algeria, kimetua Dar es Salaam, usiku wa kuamkia juzi kwenda kucheza na Young Africans ya Dar es Salaam, katika mchezo wa nne wa hatua ya Nane Bora kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaofanyika Jumamosi Agost 13, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Licha ya kwamba Young Africans ina pointi moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za juu katika kundi lao A ambalo vinara wao ni TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, zikiwa na pointi tano kila moja. Wakati Young Africans wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria, Medeama itakipiga na TP Mazembe.
Mchezo wa Young Africans dhidi ya Mo Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia huku kamishna wa mchezo akiwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda na Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan.

No comments:

Post a Comment