Monday, 15 August 2016

MESSI KUKIPIGA TENA ARGENTINA

Image result for lionel messi
Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi amekubali kurejea katika kikosi cha timu yake ya taifa ya Argentina.
Messi alitangaza kustaafu mwezi Juni baada ya michuano ya Copa America walipofungwa na Chile.
Lakini mazungumzo yaliyohusisha hadi serikali ya Argentina, yalikuwa yakiendelea na mwisho ametangaza kwamba anarejea.
  Image result for lionel messi
Ingawa hajasema moja kwa moja lakini inaelezwa ataanza kuitumikia tena Argentina katika mechi dhidi ya Uruguay halafu Venezuela kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Messi aliifungia timu yake ya taifa ya Argentina magoli 55 katika mechi 133.

No comments:

Post a Comment