Friday, 19 August 2016

MAAJABU YA SAYARI YA MARS

Image result for marsImage result for mars
Sasa Mars ni sayari kavu ambapo upepo wenye mchanga unavuma siku zote, lakini shahidi nyingi zimethibitisha kuwa katika miaka zaidi ya bilioni 3 iliyopita, ilikuwa na bahari kubwa. Lakini wakati huo iliwahi kushambuliwa na nguvu kubwa isiyojulikana ambayo ukubwa wa nguvu hii ni karibu sawa na mgongano wa sayari mbili ndogo, na kusababisha tsunami kubwa ambayo ni kubwa kuliko ile iliyotokea mwaka 2004 nchini Indonesia.
Picha zilizopigwa na satilaiti ya uchunguzi wa sayari ya Mars ya Odyssey iliyorushwa na NASA inaonesha kuwa baadhi ya sehemu za ukanda wa pwani wa bahari ya kale zimepotea, na hii hakika si hali ya awali ya bahari hiyo.
Mwanasayansi wa kituo cha fizikia ya anga cha Madrid, Hispania Bw. Alberto Fairen na kikundi chake wametafiti picha zilizopigwa na satilaiti za Odyssey na MRO za NASA, na kugundua kuwa hali ya hivi sasa ya ukanda wa pwani ni tokeo la tsunami kubwa.
Waligundua kuwa barafu na mawe viliwahi kwenda juu kwa kilomita mia kadhaa kutoka chini, hali hii huenda ilisababishwa na tsunami mbili, ambayo ya kwanza ilipeleka miamba yenye upana wa mita kadhaa katika sehemu ya juu, na ya pili iliyotokea katika siku ya baridi ilipeleka barafu juu.
Kompyuta imekadiria kuwa mgongano wa sayari ndogo unaweza kusababisha shimo lenye kipenyo cha 30, na mawimbi ya baharini yaliyosababishwa na mgongano huo yakifika pwani, urefu wake utafikia mita 50.

No comments:

Post a Comment