Nyota wa tenisi Novak Djokovic ameshindwa kwenye raundi ya kwanza katika mashindano ya mchezaji mmoja mmoja michezo ya Olimpiki Rio inayoendelea nchini Brazil.
Nyota huyo raia wa Serbia Djokovic alishindwa na raia wa Argentina Juan Martin Del Potro.
Djokovic mwenye umri wa miaka 29 ambaye ndiye mchezaji bora duniani, alitokwa na machozi akiondoka uwanjani baada ya mchezo huo uliodumu kwa saa mbili na nusu.
No comments:
Post a Comment