Tuesday, 9 August 2016

WEST HAM UNITED YAMSAJILI ANDRE AYEW KWA UERO MILIONI 20.5

Image result for andre ayew
Klabu ya West Ham United imekamilisha usajili wa fowadi wa Swansea City Andre Ayew kwa dau la euro milioni 20.5.
Ayew, mwenye umri wa miaka 26 alikuwa amehamia Swansea bila malipo akitokea Marseille mwezi Juni 2015 na kufunga mabao 12 kwenye msimu wa kwanza wa ligi kuu.
  Image result for andre ayew
Sasa Ayew ambaye ni raia wa Ghana anasaini mkataba wa miaka 4 na West Ham na amekuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na kblabu hiyo msimu huu.
Sofiane Feghouli, Havard Nordtveit na Ashley Fletcher tayari wamesaini kwa uhamisho usiokuwa wa malipo.

No comments:

Post a Comment