Sunday, 7 August 2016
PATASHIKA UHAKIKI WA VYETI,ZAMU YA SENGEREMA
Mkurugenzi wa halimashauri ya sengerema MAGESA BONIFACE amewataka watumishi wa halimashauri hiyo wajiandae kuhakikiwa vyeti vyao vya kitaaluma.Akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo katika kikao cha kujitambulisha na kuelezea mikakati yake.
Magesa amesema kazi hyo itaanza kutekelezwa wilayani humo kuanzia septemba mosi mwaka huu,"kila mtu anatakiwa kuandaa na kuwasilisha vyeti halisi vya kitaaluma walivyotumia kupata fursa za ajira walizonazo",alisema mkurugenzi huyo na kuagiza wakuu wa idara kusimamia kazi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment