Monday, 15 August 2016
JANUZAJ ATUA SUNDERLAND KWA MKOPO
Winga wa Manchester United Adnan Januzaj, amejiunga na sunderland kwa mkopo msimu huu wa 2016/17.
Uhamisho huo umemuunganisha na meneja wake wa zamani David Moyes pamoja na wachezaji weza Donald Love na Paddy McNair aliyejiunga na timu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 5.5 wiki hii.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ubeligiji, Januzaj, alikuwa anataka kutoka Old Trafford kabisa lakini klabu
hiyo ya United iliamua kumkabidhi kwa klabu hiyo kwa mkopo.
Januzaj alifunga mabao matano katika mechi 63 alizoshiriki kwenye klabu ya United.
Mkataba wake na Manchester United utamalika mwaka 2018.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment