Monday, 22 August 2016

TFF YAFUNGIA WATANO LIGI KUU

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho la kandanda nchini Tanzania TFF imewafungiwa wachezaji watano kutoka klabu tano zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Shirikisho limetoa tahadhari kwa klabu za Mbeya City, Majimaji, Mwadui FC, Mbao FC na African Lyon kutowatumia wachezaji hao, kwani watatu wamefungiwa mwaka mmoja na wawili wamesimamishwa kwa juma moja.
Lucas alisema wachezaji hao wamegundulika kufanya udanganyifu huo kupitia usajili ambao wamefanya hapo awali kwani sura za kwenye picha ni ile ile, lakini majina ndio yamebadilishwa.

No comments:

Post a Comment